Breaking


Jumatano, 27 Mei 2026

PPP YALETA MAPINDUZI HUDUMA ZA HIJJA MAKKA-KAFULILA

Mkurugenzi Mtendaji wa PPP-Centre, David Kafulila, amesema mfumo wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na sekta Binafsi-PPP, umeleta mageuzi katika huduma za Hijja nchini Saudi Arabia kwa kuongeza ufanisi na kupunguza adha kwa Mahujaji.

Akitoa salamu za Eid al-Adha kwa Waislamu duniani, Kafulila amesema moja ya mafanikio makubwa ya PPP ni maboresho yaliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa King Abdulaziz-KAIA uliopo Jeddah, unaotumiwa na mamilioni ya mahujaji wanaoelekea Makka.

Kabla ya maboresho hayo, mahujaji walikuwa wakitumia kati ya saa sita hadi 10 kukamilisha taratibu za uwanjani, lakini baada ya utekelezaji wa mradi wa PPP wenye thamani ya dola milioni-249, muda huo umepungua hadi dakika 45 na saa moja.

Mradi huo ulitekelezwa kupitia mkataba wa miaka 20 kati ya Mamlaka ya Anga ya Saudi Arabia-GACA na kampuni binafsi ya Hajj and Umrah Terminals Development Company, ukihusisha Saudi Binladin Group pamoja na Aéroports de Paris Management huku Shirika la IFC likiwa mshauri mwelekezi na kwamba mafanikio hayo yanapaswa kuwa somo kwa Tanzania katika kuendeleza sekta ya usafiri wa anga na miundombinu mingine kupitia uwekezaji wa PPP.

Aidha, Kafulila, amesema tathmini ya usafiri wa anga duniani ya mwaka 2023 inaonyesha kuwa licha ya viwanja vya ndege vinavyoendeshwa kwa PPP kuwa asilimia 14 pekee duniani, vinahudumia karibu asilimia 40 ya abiria wote duniani.

Hakuna maoni: