Mchezo huo unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka duniani kote huku timu zote mbili zikionyesha kiwango bora katika michuano hiyo msimu huu. PSG imefanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kufanya vizuri katika michezo yake ya hatua za mtoano, huku Arsenal nayo ikionesha ubora mkubwa dhidi ya wapinzani wake.
Fainali hiyo inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na ubora wa vikosi vya timu zote mbili pamoja na uwepo wa nyota wanaoweza kubadili matokeo muda wowote ndani ya uwanja.
Mashabiki wengi wameanza kufanya maandalizi ya kushuhudia pambano hilo ambalo linaelezwa kuwa moja ya michezo mikubwa zaidi ya soka barani Ulaya mwaka huu.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni