Breaking


Ijumaa, 15 Mei 2026

TAKUKURU KINONDONI YABAINI UKWEPAJI USHURU WA SERVICE LEVY

 



TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa-TAKUKURU mkoa wa kinondoni imefanikiwa kudhibiti upotevu wa mapato ya zaidi ya shilingi milioni mia tano ambapo udhibiti huo umefanyika baada ya kupokea taarifa za kuwepo kwa baadhi ya wafanyabiashara kukwepa  kulipa ushuru wa huduma yaani SERVICE LEVY.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam May 15 na Naibu Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa kinondoni  Elizabeth Mokiwa wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya utrndaji kazi wa TAKUKURU mkoa huo kwa kipindi cha January hadi Mach 2026 ambapo amesema kukwepa kulipa ushuru huo husababisha upotevu wa mapato yanayostahili kukusanywa na halmashauri na kutofikia malengo ya makusanyo yaliyotarajiwa.



Katika hatua nyingine TAKUKURU mkoa wa kinondoni imefuatilia matumizi ya fedha za utekelezaji wa miradi saba ya maendeleo, miradi mitatu ikiwa ni ya sekta ya afya yenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 1.62 na miradi minne ya sekta ya elimu yenye thamani ya shilingi milioni 340.4.

Mbali na hayo pia imefanikiwa kutoa elimu kwa umma kwa kuwafikia wananchi elfu 6,572 wakiwemo watumishi wa umma, vikundi vya kijamii, wanafunzi ,VICOBA na viongozi wa skauti wilaya ya kinondoni.



Aidha TAKUKURU Mkoa wa Kiondoni  imeweka mikakati kwa kipindi cha mwezi april hadi juni 2026 ambapo imejipanga kuendelea kufuatulia matumizi ya fedha za serikali katika miradi ya maendeleo , kuendelea kutoa elimu kwa wananchi na wadau kuhusu kuzuia rushwa kwenye miradi ya maendeleo pamoja na kuendelea kufuatilia utrkelezaji wa mapendekezo ya programu ya TAKUKURU-Rafiki

Hakuna maoni: