Breaking


Ijumaa, 8 Mei 2026

TANZANIA NA ZAMBIA ZAJADILI KUKUZA BIASHARA

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), ameshiriki Mkutano wa Tano wa Kamati ya Pamoja ya Biashara (5th Joint Trade Committee - JTC) kati ya Tanzania na Zambia, uliofanyika Mjini Tunduma, Mpakani mwa Tanzania na Zambia, katika Mkoa wa Songwe, ambapo wamejadili kwa kina namna ya kukuza biashara kwa faida ya nchi hizo mbili.

Katika mkutano huo pande zote mbili zilijadili kuhusu namna ya kuboresha mazingira ya biashara na miundombinu yake ikiwemo sekta ya usafirishaji itakayochochea ufanyaji biashara na kutoa fursa zaidi kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa nchi zote mbili.

Mkutano huo ulitanguliwa na kikao cha ngazi ya Wataalamu, na kufuatiwa na kikao cha ngazi ya Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali ikiwemo Wizara ya Fedha, Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Viwanda na Biashara Pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Zambia.


Viongozi wengine wa Serikali ya Tanzania walioshiriki Mkutano huo ni Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile (Mb), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. James Millya (Mb), Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Denis Londo (Mb), pamoja na viongozi wengine waandamizi kutoka Serikali ya Zambia.

Hakuna maoni: