Breaking


Ijumaa, 8 Mei 2026

MMILIKI WA KAMPUNI KUBWA YA UTALII DUNIANI YA ABERCROMBIE AND KENT KUWEKEZA ZAIDI TANZANIA


Bilionea na mmiliki wa moja ya kampuni kubwa zaidi duniani katika biashara ya utalii ya Abercrombie and Kent, Bw. Manfred Lefebvre amesifu maendeleo ya sekta ya utalii nchini Tanzania na kuahidi kuwekeza zaidi nchini.

Bw. Manfred ameyasema hayo katika magungumzo leo Ijumaa Mei 8, 2026 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii nchini Tanzania, Dkt. Hassan Abbasi, pembeni mwa Mkutano wa Viongozi wa Sekta unaofanyika ndani ya meli ya kitalii ya bilionea huyo ambayo leo inaendelea na safiri kutoka Bandari ya Port Said kwenda Alexandria. 

“Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo naziona zikiendelea vyema katika sekta ya utalii barani Afrika. Nauona uongozi wa sasa ukiweka mbele utalii sana hasa chini ya Rais Mama Samia,” alisema Bw. Manfred ambaye miaka minne iliyopita pia alihudhuria uzinduzi wa filamu ya “Tanzania: The Royal Tour,” jijini New York, Marekani. 

Kampuni ya Abercrombie and Kent tayari imewekeza Tanzania ikileta maelefu ya watalii wakiwemo wale wanaofika nchini kupitia meli zao za kitalii chini ya kampuni tanzu ya Crystal Cruises ambazo huvinjari mara kadhaa Zanzibar, Kilwa na Dar es Salaam. 

Kwa upande wake Dkt. Abbasi alimhakikisha ushirikiano na Serikali katika hatua zake zote zijazo za kuongeza wigo wa uwekezaji wake nchini Tanzania.

Hakuna maoni: