Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Mbelwa Brighton Kairuki, amelipongeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na Ofisi ya Ubalozi katika kuiwakilisha Tanzania kwenye Kikao cha Mfuko wa Fidia wa Kimataifa wa Kukabiliana na Uchafuzi wa Bahari unaosababishwa na kumwagika kwa mafuta baharini (IOPC Funds), kilichofanyika jijini London, Uingereza.
Mheshimiwa Balozi amemshukuru na kumpongeza Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware Semesi, kwa kuanza kutuma wataalamu wa NEMC kushiriki katika vikao mbalimbali vinavyoandaliwa na (IMO), akieleza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kuiwezesha Tanzania kuendelea kushiriki kikamilifu katika masuala ya Usimamizi wa Mazingira ya bahari katika ngazi ya kimataifa.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa NEMC kuendelea kushiriki katika majukwaa hayo ya kimataifa ili kujenga uwezo wa wataalamu wa Tanzania, kubadilishana uzoefu na kuhakikisha nchi inanufaika na mifumo ya kimataifa ya kulinda mazingira na usalama wa bahari.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni