Akijibu swali bungeni jijini Dodoma Mei 26, 2026, Waziri huyo alisema Serikali inaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia sekta ya mifugo na uvuvi.
Kauli hiyo ilitolewa wakati akijibu swali la Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Amos Bulaya, aliyehoji ni lini vijana wa Bunda watanufaika na Mradi wa Ufugaji wa Samaki kwa Vizimba unaosimamiwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Kwa mujibu wa Waziri Bashiru, Wizara hiyo kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI pamoja na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania ilitangaza Machi 4, 2026 fursa ya mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 23.68 kwa ajili ya vijana wanaojishughulisha na sekta za mifugo na uvuvi.
Alisema maombi hayo yametoka maeneo mbalimbali nchini, yakiwemo kutoka Wilaya ya Bunda, na kwamba uchambuzi unaendelea ili kubaini waombaji waliokidhi vigezo vya kupata mikopo hiyo.
Aidha, Waziri Bashiru alisema katika mwaka wa fedha 2025/2026 Serikali ilitekeleza awamu ya kwanza ya utoaji wa mikopo ya vizimba vya kufugia samaki kwa vijana ambapo jumla ya vizimba 95 vilitolewa katika Mkoa wa Mara Region, huku vizimba 20 vikielekezwa Wilaya ya Bunda.
Pamoja na hayo, Waziri huyo aliitaka Halmashauri ya Mji wa Bunda kuelekeza sehemu ya mikopo ya asilimia 10 ya vijana kwenye shughuli za ufugaji wa samaki kwa vizimba ili kuongeza ushiriki wa vijana katika kukuza uchumi wa buluu nchini.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni