Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amefanya mazungumzo na Watanzania wanaoongoza mashirika ya kikanda na kimataifa kando ya Mkutano wa 61 wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), unaoendelea jijini Brazzaville, Jamhuri ya Kongo Jumatano Mei 27, 2026.
Katika mazungumzo hayo, Dkt. Mwigulu alikutana na Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika (WHO AFRO), Prof. Mohamed Janabi ambapo walijadili masuala mbalimbali ya maendeleo, hususan ushirikiano katika sekta ya afya barani Afrika.
Aidha, Waziri Mkuu alifanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi ambapo walijadili masuala ya kuimarisha ushirikiano wa kikanda pamoja na utekelezaji wa miradi ya pamoja ya maendeleo inayolenga kukuza biashara, uwekezaji na miundombinu ndani ya Jumuiya hiyo.Pia, Dkt. Mwigulu alikutana na Katibu Mkuu wa Jukwaa la Mabunge ya Ukanda wa Maziwa Makuu Afrika (FP-ICGLR), Balozi Dkt. Deo Mwapinga ambapo walibadilishana mawazo kuhusu masuala ya amani, usalama na maendeleo katika ukanda wa Maziwa Makuu Afrika.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni