Breaking


Jumatano, 3 Juni 2026

BEI YA PETROLI YASHUKA NCHINI TANZANIA

Watumiaji wa nishati ya Petroli wamepata afueni mwezi huu, baada ya bei ya mafuta hayo kushuka ikilinganishwa na mwezi uliopita. 

Kwa Dar es Salaam, Petroli inauzwa kwa bei kikomo ya shilingi 4,086 kwa lita moja, hatua inayotarajiwa kupunguza gharama kwa watumiaji wa kawaida na baadhi ya shughuli za usafiri.

Kwa upande wa dizeli, watumiaji wanakabiliwa na ongezeko dogo la bei, ambapo jijini Dar es Salaam bei kikomo imefikia shilingi 4,333 kwa lita moja, na mafuta ya taa shilingi 4,685 kwa lita.

Kwa mujibu wa EWURA, ongezeko hilo limechangiwa na kupanda kwa gharama za mafuta katika soko la dunia, pamoja na kuongezeka kwa gharama za uagizaji wa bidhaa hiyo.

Licha ya changamoto hizo za kimataifa, Serikali imeendelea kuchukua hatua za kulinda uchumi na wananchi kwa kuweka ruzuku ya shilingi 535 kwa kila lita ya dizeli. 

Aidha, hali hiyo inaathiriwa na vita vinavyoendelea katika Mashariki ya Kati, vinavyohusisha Marekani, Israel na Iran.

Hakuna maoni: