Breaking


Jumanne, 23 Juni 2026

BEYONCÉ AFUNGUKA ZAIDI

Mwimbaji maarufu duniani, Beyoncé, ameshiriki simulizi ya kuvutia kuhusu jinsi binti yao alivyochangia mabadiliko ya mwonekano wa baba yake, Jay-Z.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Beyoncé alisema kuwa binti yao alikuwa na umri wa takriban miaka mitano wakati alipokuwa akikosa kujiamini kuhusu nywele zake. Alipomweleza baba yake hali hiyo, Jay-Z alipata msukumo wa kukuza nywele zake kama njia ya kumuonyesha sapoti na kumjengea kujiamini.

“Binti yetu alikuwa na umri wa karibu miaka mitano na hakuwa anajiamini sana kuhusu nywele zake wakati huo. Alipomwambia baba yake kuhusu hilo, jambo hilo lilimpa Jay msukumo wa kukuza nywele zake,” alisema Beyoncé.

Kauli hiyo imeibua mijadala mitandaoni, huku wengi wakisifu namna wazazi wanavyoweza kutumia matendo yao kuwajengea watoto kujiamini na kujikubali walivyo.

Hatua ya Jay-Z inaonekana kuwa mfano wa jinsi familia inaweza kusaidiana katika kujenga hali ya kujiamini kwa watoto, hasa katika kipindi cha ukuaji ambapo taswira binafsi huwa na mchango mkubwa katika maendeleo yao ya kihisia na kijamii.

Wafuasi wa familia hiyo wameeleza kuwa simulizi hilo linaonyesha umuhimu wa upendo, uelewa na msaada wa wazazi katika kuwasaidia watoto kukabiliana na changamoto za kujiamini.


Hakuna maoni: