Breaking


Jumatano, 3 Juni 2026

MAOFISA MAWASILIANO WATAKIWA KUSIMULIA MAFANIKIO YA MIRADI YA SERIKALI



Maofisa Uhusiano na Mawasiliano Serikalini wametakiwa kutengeneza simulizi zenye mvuto na tafsiri sahihi zitakazowasaidia wananchi kuelewa fursa mbalimbali zinazotekelezwa na Serikali kupitia miradi ya maendeleo nchini.

Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa, wakati akiwasilisha mada kuhusu “Miundombinu kama Mhimili wa Ajira, Biashara, Huduma na Ushindani wa Taifa”katika  Mkutano wa Mwaka wa Chama cha Maofisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) unaoendelea jijini Mwanza.

Bw. Msigwa amesema maofisa mawasiliano wanapaswa kutumia ubunifu na maarifa yao kueleza kwa wananchi mafanikio makubwa yaliyopatikana kupitia uwekezaji wa Serikali katika sekta ya miundombinu.

“Sekta hii ni muhimu na ina mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa. Mna jukumu la kujenga uhusiano mzuri kati ya Serikali na wananchi

Hakuna maoni: