Breaking


Ijumaa, 12 Juni 2026

MASHABIKI TANZANIA KUNUFAIKA NA KAMPENI MAALUM YA KOMBE LA DUNIA


wanatarajiwa kupata fursa ya kushiriki kikamilifu katika shamrashamra za Kombe la Dunia la FIFA 2026™️ kupitia kampeni maalum ya kitaifa itakayofanyika kuanzia Juni 11 hadi Julai 19, 2026. Kampeni hiyo itajumuisha burudani mbalimbali, matangazo maalum kwenye maduka na shughuli za kidijitali zitakazolenga kuwaleta mashabiki karibu zaidi na msisimko wa michuano hiyo.

Kupitia kampeni hiyo, wateja watapata nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali, kufurahia burudani za kipekee na kupata bidhaa zenye nembo maalum ya Kombe la Dunia la FIFA 2026™️, ikiwemo vinywaji na mikoba ya kumbukumbu iliyotengenezwa mahsusi kwa ajili ya mashindano hayo.

Kampuni ya Coca-Cola Tanzania imesema kampeni hiyo inalenga kuunganisha mashabiki wa soka kote nchini na kuwapa fursa ya kusherehekea kila hatua ya michuano hiyo kupitia maeneo mbalimbali ya huduma, maduka ya rejareja, migahawa na vituo vya vyakula. Kampuni hiyo ina historia ya takriban miaka 50 ya ushirikiano na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Mkurugenzi wa Masoko wa Coca-Cola Tanzania, Kabula Nshimo, amesema soka ni zaidi ya mchezo kwani lina uwezo wa kuwaunganisha watu kupitia hisia za pamoja zinazojitokeza wakati wa Kombe la Dunia. Amesema kampeni hiyo inalenga kugeuza furaha ya ushindi na simanzi ya kufungwa kuwa fursa za kujenga mahusiano na mshikamano miongoni mwa mashabiki.

Hakuna maoni: