Nyota huyo raia wa Brazil, ambaye amekuwa miongoni mwa wachezaji muhimu wa Fulham katika msimu uliopita wa Ligi Kuu ya England (EPL), amechagua Tanzania kama moja ya maeneo yake ya kutembelea wakati wa likizo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Muniz alichapisha picha zikimuonyesha akiwa katika gari la utalii ndani ya Serengeti National Park, moja ya vivutio vikubwa vya utalii nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla.Pamoja na picha hizo, mshambuliaji huyo aliandika ujumbe mfupi wa “African Vibes!” na kuweka emoji ya bendera ya Tanzania, jambo lililovutia mashabiki wake pamoja na wadau wa soka na utalii.
Ziara ya Muniz inaendelea kuonyesha jinsi Tanzania inavyozidi kuwa kivutio cha watalii na watu maarufu kutoka mbalimbali duniani, hasa kutokana na hifadhi zake za wanyamapori, mandhari za asili na urithi wake wa kipekee wa utalii.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni