Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) yaendelea kuwajengea uelewa wananchi juu ya masuala mbalimbali ya hali ya hewa kupitia maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Chinangali Park, Jijini Dodoma kuanzia Tarehe 16 – 23 Juni 2026.
Maadhimisho hayo yalifunguliwa rasmi tarehe 17 Juni 2026 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete, na yanatarajiwa kufikia kilele chake tarehe 23 Juni 2026.
Katika maonesho hayo, wananchi wameendelea kukaribishwa kutembelea banda la TMA ili kutumia fursa hiyo kujifunza namna ya kuzitafsiri taarifa za hali ya hewa pamoja na matumizi sahihi kwa sekta husika ikiwemo kilimo, usafiri na uvuvi, hatua itakayosaidia kuongezeka kwa ufanisi katika shughuli za kimaendeleo.
Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni: “Kuchochea uwajibikaji jumuishi kwa huduma endelevu.”




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni