Wabunge wamezipongeza NSSF na PSSSF kwa juhudi zao za kuimarisha ustawi wa wananchi kupitia Skimu ya Hifadhi ya Jamii kwa Wananchi Waliojiajiri na uwekezaji katika Kiwanda cha Kimataifa cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro (KLICL).
Akifungua semina maalum kwa wabunge jijini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano ya Kazi, Deus Sangu, amesema Serikali imejipanga kuhakikisha wananchi waliojiajiri wananufaika na huduma za hifadhi ya jamii kama ilivyo kwa wafanyakazi wa sekta rasmi.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, amesema skimu hiyo inalenga kuwafikia mamilioni ya Watanzania waliojiajiri kupitia mfumo rahisi wa usajili na uchangiaji wa kidijitali, huku wanachama wakinufaika na mafao mbalimbali ya hifadhi ya jamii.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Fortunatus Magambo, amesema Kiwanda cha Kimataifa cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro kimechangia kuongeza ajira, kukuza viwanda na kuimarisha soko la ngozi kwa wafugaji nchini.
Wabunge walioshiriki semina hiyo wameeleza kuridhishwa na hatua hizo, wakisema zitasaidia kuongeza ushiriki wa wananchi katika hifadhi ya jamii na kuchochea maendeleo ya viwanda na uchumi wa taifa.





Hakuna maoni:
Chapisha Maoni