Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Ridhiwani Kikwete amewataka wanafunzi wanasoma masomo ya Sheria kuhakikisha wanajenga na kuimarisha taaluma zao katika misingi ya nidhamu, ubunifu na uzalebdo.
Waziri Ridhiwani amesema hayo wakati akizungumza na wanafunzi Wanasheri, katika Siku ya Kazi na Taaluma ya shule ya Sheria na kufanyika kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Amesema kwamba wanafunzi hao wakiwa wabunifu na wazalendo wataweza kuleta mafanikio makubwa katika soko la ajira la kimataifa ambapo kwa hivi sasa ndiyo ulishindani uliyopo.
Katika hafla ya Siku ya Kazi na Taaluma ya Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, nimezungumza na kuwataka Wanafunzi wa sheria kujenga taaluma zao katika misingi ya nidhamu, ubunifu na uzalendo ili waweze kufanikiwa katika soko la ajira la kimataifa linalozidi kuwa na ushindani.
Aidha amewakumbusha wanafunzi hao kwa kuwaambia Serikali ya awamu ya Sita, chini ya Rais Dokta Samia Suluhu Hassan imeweza kuimarisha sekta ya Sheria na Haki kupitia mageuzi ya teknolojia, uwekezaji pamoja na miundombinu ya utoaji haki kwa ujumla.
Katika hotuba yangu nimewakumbusha kuwa mafanikio ya Taalum leo, hayawezi kupatikana bila kuzingatia kuwa taalum zetu zinatutaka kutengeneza uwezo wa kushindana nje ya mipaka yetu huku maadili haswa nidhamu, Uzalendo na ujuzi katika sheria ni moja ya Jambo muhimu sana kuzingatiwa.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni