Picha zake zimekuwa zikisambaa kwa kasi mtandaoni, huku watumiaji wengi wakisifu sura yake na ngozi yake ya asili. Umaarufu wake unaendelea kuongezeka, na kuzua mjadala kuhusu nafasi anayoweza kupata katika sekta ya mitindo na urembo.
Kwa mujibu wa taarifa zinazosambaa mtandaoni, kuna wadau wa sekta ya mitindo wanaoonyesha nia ya kumsaidia Elisabeth kupata fursa zaidi, ikiwemo kumhamishia jijini Addis Ababa ili aweze kuendeleza vipaji na ndoto zake katika tasnia hiyo. Hata hivyo, taarifa kuhusu ushirikiano rasmi na makampuni makubwa ya kimataifa bado hazijathibitishwa rasmi.Iwapo atapata fursa hizo, safari ya Elisabeth inaweza kuwa mfano wa jinsi vipaji na mwonekano wa kipekee vinavyoweza kufungua milango ya mafanikio, hata kwa watu wanaotoka maeneo ya vijijini.
Je, unadhani Elisabeth Desta anaweza kuwa mmoja wa nyota wapya wa kimataifa katika ulimwengu wa mitindo? Toa maoni yako.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni