Katika taarifa yake kwa umma, Jeshi la Polisi limeeleza kuwa kwa nyakati tofauti limekuwa likitoa taarifa kuhusu masuala ya kiusalama, ikiwemo taarifa zinazohusu baadhi ya watu wanaodaiwa kupanga na kuhamasisha vitendo vinavyokiuka sheria kwa kutumia maandamano yasiyofuata taratibu za kisheria.
Jeshi la Polisi Tanzania limesema hali ya usalama nchini inaendelea kuwa shwari na kuwahakikishia wananchi kuwa litaendelea kupokea taarifa za nia ya kufanya mikutano kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zinazotumika nchini.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni