Kwa mujibu wa taarifa za maafisa wa afya zilizoripotiwa na shirika hilo, waliopoteza maisha ni baba, mama na mtoto wao mwenye umri wa miaka miwili baada ya nyumba yao iliyopo eneo la Chahtangu, mjini Qeshm, kulengwa katika shambulizi hilo.
Aidha, kwa mujibu wa BBC Persian, watoto wengine wawili waliokuwa ndani ya nyumba hiyo walijeruhiwa na wamepelekwa hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Hadi wakati wa kuchapishwa kwa taarifa hii, mamlaka husika hazijatoa taarifa zaidi kuhusu mazingira ya tukio hilo, huku taarifa kutoka pande mbalimbali zikiendelea kufuatiliwa ili kubaini undani wa kilichotokea.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni