Katika picha hizo, A$AP Rocky anaonekana akitumia muda pamoja na watoto wake, huku akiwa amembeba mmoja mabegani, mwingine mikononi na kubeba pia baadhi ya vitu vya familia.
Muonekano huo umeonyesha upande mwingine wa maisha ya msanii huyo nje ya muziki, akionekana kuwa baba anayeshiriki kikamilifu katika malezi na kutumia muda wa karibu na watoto wake.
Picha hizo zimevutia hisia za mashabiki, huku wengi wakisifu namna A$AP Rocky anavyoonekana kuwa karibu na familia yake na kufurahia majukumu ya ubaba.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni