Kiungo wa Aziz Ki amepata pigo baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Geita Gold.
Kutokana na adhabu hiyo, Aziz Ki anatarajiwa kukosa michezo miwili ijayo ya Ligi Kuu, jambo linaloweza kuwa changamoto kwa timu yake katika kipindi hiki muhimu cha msimu.
Kwa mujibu wa ratiba, moja ya michezo ambayo kiungo huyo anaweza kukosa ni mchezo dhidi ya Simba SC.
Kutokuwepo kwa Aziz Ki kunaweza kuathiri mipango ya kikosi, hasa kutokana na umuhimu wake katika eneo la kiungo na mchango wake katika kutengeneza nafasi za kufunga.
Mashabiki sasa wanasubiri kuona namna benchi la ufundi litakavyomziba pengo lake katika michezo hiyo miwili.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni