Breaking


Jumanne, 1 Septemba 2026

IBRAHIM DOUMBIA AWASHUKURU MASHABIKI WA SIMBA: “SIMBA NGUVU MOJA!”

Mchezaji wa Simba SC, Ibrahim Doumbia, amewashukuru mashabiki wa klabu hiyo kwa upendo, sapoti na uvumilivu wanaomuonyesha, akisema kuwa wameendelea kuwa pamoja naye katika kipindi ambacho amekutana na changamoto mbalimbali.

Doumbia ameeleza kuwa aliguswa sana baada ya kushuka kwenye basi na kuona bango lenye ujumbe wa mashabiki lililoandikwa, “WE ARE TOGETHER DOUMBIA. WE LOVE YOU.”

Mchezaji huyo amesema tukio hilo lilimfanya ahisi hisia kubwa na hata kutokwa na machozi, akisisitiza kuwa katika soka kuna nyakati za ushindi, kushindwa, kukosolewa na kuwa na mashaka, lakini sapoti ya mashabiki imemkumbusha kuwa hayuko peke yake.

“Kwa mashabiki wote wa Simba, tafadhali mjue kwamba bila kujali kitakachotokea, tayari mpo moyoni mwangu. Nahisi upendo, sapoti na imani yenu,” alisema Doumbia.

Amesema anaendelea kujituma ili kuilinda na kuiheshimisha jezi ya Simba, huku akiamini kuwa changamoto wanazopitia wataweza kuzivuka kwa pamoja.

Doumbia pia amewashukuru mashabiki waliokuwa wakimpa moyo, kumuombea na kumuamini, pamoja na wale wanaomkosoa.

Kwa mujibu wa mchezaji huyo, hata ukosoaji unaweza kuwa sehemu ya nguvu inayomsukuma kufanya kazi kwa bidii zaidi na kuboresha kiwango chake.

“Sitaki kuzungumza sana. Nataka kufanya kazi, kujifunza, kuboresha, kupambana na zaidi ya yote, nataka kulipa upendo wenu ndani ya uwanja,” amesema.

Doumbia amesisitiza kuwa anaamini nyakati bora bado ziko mbele yake na amewataka mashabiki kuendelea kuwa pamoja naye.

Katika ujumbe wake wa mwisho, amewashukuru mashabiki wa Simba kwa upendo, uvumilivu na sapoti yao, akihitimisha kwa kauli:

“I LOVE YOU ALL. SIMBA NGUVU MOJA!”

Baada ya mchezo huo, Doumbia pia alieleza kuwa aliguswa na makofi ya mashabiki, akisema kuwa licha ya changamoto zilizokuwepo, mashabiki waliendelea kuwa upande wake na jambo hilo lilimfurahisha.


Hakuna maoni: