WAZIRI wa Viwanda na Biashara Mhe.Judith Kapinga (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa nchi anayeshughulikia Shirikisho la Ulaya na Kimataifa mwenye dhamana ya kuratibu tatatibu za kiutawala jimbo la Hessen kutoka shirikisho la nchi ya Ujerumani Mhe. Manfred Pentz aliyeambatana na wafanyabiashara na wawekezaji takribani 30 kutoka nchini humo.
Akizungumza wakati wa mazungumzo na Ujumbe huo wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka ujerumani Mhe Kapinga amesema, kwa sasa Tanzania imejikita kwenye kuongeza mnyororo wa thamanini kwa mazao mbalimbali ikiwemo yale ya usindikaji kwenye mazao ya kilimo, mbolea, madawa, hapa nchini ili kuongeza thamani.
Aidha Mhe Kapinga aliongeza kuwa, chini uongozi wa Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, nchi ya Tanzania imejipanga kufikia uchumi wa Dola Trilioni 1 ifikapo mwaka 2050 na kuhakikisha mauzo ya nje yanaongezeka.
Kwa upande wake Waziri wa nchi anayeshughulikia shirikisho la Ulaya na kimataifa mwenye dhamana ya kuratibu taratibu za kiutawala Jimbo la Hessen Mhe. Manfred Pentz amesema, Tanzania ina fursa nyingi na maeneo ya kuwekeza kwenye sekta ya Kilimo, Madawa Utalii na gesi na mafuta na ujerumani iko tayari kushirikiana nayo kwenye maeneo hiyo kutokana na uwepo wa sera rafiki za Uwekezaji.
Ameitaka Tanzania kutumia fursa kwenye mkutano wa jukwaa la kibiashara itakaofanyika mwezi Februari mwakani kushiriki na kunadi fursa za nchi ili kuvutia wawekezaji wengi zaidi kutoka nchini ujerumani.
Jumla ya wawekezaji takribani 30 kutoka nchini ujerumani wako hapa nchini kuangalia fursa za uwekezaji kwa Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania na kuimarisha ushirikiano baina ya pande hizi mbili Kati ya Tanzania na Ujerumani.
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Naibu katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Aristides Mbwasi, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani na Wakurugenzi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara na wawakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki.






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni