Rasmi klabu ya Chelsea ya nchini England imetwaa ubingwa wa kombe la dunia la FIFA ngazi ya vilabu (FIFA Club World Cup) kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya mabingwa wa Ulaya (Uefa Champions League) ,Paris St-Germain ya nchini Ufaransa kwenye mchezo wa fainali uliyopigwa katika dimba la MetLife, New Jersey nchini Marekani.
Chelsea inatwaa kombe hilo kwa mara ya pili (2) baada ya kufanya hivyo mnano mwaka 2021 na ikiwa pia ni taji lake la pili msimu huu baada ya kubeba ubingwa wa UEFA Conference League.
Kipigo hicho kimeikosesha PSG kombe la tano (5) msimu huu baada ya kutwaa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Ligue 1, Couple De France na France Super Cup.
Kwenye mchezo wa leo wa fainali mabao hayo matatu kwa Chelsea yamefungwa na Cole Palmer mawili dakika yq 22 na dakika ya 30 pamoja na goli la Joao Pedro dakika ya 43 ya mchezo na kuhitimisha kalamu hiyo ya mabao 3-0 dhidi ya PSG ambaye ndio bingwa ligi ya mabingwa ulaya.
✍🏾 AnoldMathias255

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni