Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuzindua Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inahitajika kuelekeza nguvu katika vitendo zaidi kuliko maneno ili kufikia mafanaiko
Aidha Rais Samia amesema dira ya Taifa ya maendeleo 2050 imezingatia muktadha wa dunia ya leo iliyojaa mabadiliko makubwa na changamoto zisizotabirika sambamba na dunia yenye fursa nyingi.
Amesema lengo lililowekwa ni kuwa taifa jumuishi lenye ustawi haki na linalojitegemea.
Ametaka Serikali, sekta binafsi na wananchi kutenda zaidi kuliko kusema huku akisema mtuhani zaidi ni katika utekelezaji ili kufikia lengo.
Rais Samia amesema hayo leo Jijini Dodoma alipokuwa akizindua Dira ya Taifa ya maendeleo 2050, huku akisema Dira hiyo inavipaumbele ikiwemo Sekta ya Kilimo, utalii, Viwanda, Ujenzi, madini, Uchumi wa buluu



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni