Breaking

Jumapili, 13 Julai 2025

HAKUNA ALIYEKATWA, UTEUZI WA MWISHO KUFANYWA NA KAMATI KUU- MAKALLA.

 

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimesema hadi sasa hakuna mwanachama  aliyekatwa, kufyekwa au kuenguliwa jina lake  katika mchakato wa uteuzi wa wagombea wa ubunge, uwakilishi na udiwani hadi pale Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya chama hicho itakapokamilisha kazi yake.

Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla ameyasema hayo leo Julai 13,2025, jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanza kwa vikao vya CCM ngazi ya Taifa.

"Katika ngazi ya Kitaifa leo tumeanza na sekretarieti ya CCM kupokea taarifa kutoka mikoa mbalimbali ili na sisi tuweze kuziratibu na kuziwekea utaratibu wa kuelekea vikao vikubwa vya juu vya uteuzi kwa maana ya Kamati Kuu, hivyo tunaendelea kuzifanyia kazi taarifa hizo,

"Kwa utaratibu wetu na mchakato ndani ya ya CCM,mpaka sasa hakuna mtu ambaye ameenguliwa,kukatwa ama kufyekwa,nimeona huyu kapenya,huyu kafyekwa,huyu hayumo kwenye tatu bora,nawaambia mchakato wa uteuzi utahitimishwa na Kamati Kuu,".amesema.

Makalla amewaasa watia nia kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho mchakato bado unaendelea hadi pale Kamati kuu itakapotoa uamuzi wa mwisho.

Hakuna maoni: