Breaking


Ijumaa, 25 Julai 2025

HARUSI YA SIRI, TALAKA YA HARAKA: TONI BRAXTON NA BIRDMAN

 

Mwanamuziki mashuhuri wa R&B, Toni Braxton, na rapa mkongwe Birdman wametikisa vichwa vya habari baada ya kufichuka kuwa walifunga ndoa kwa siri mwezi Agosti 2024, lakini ndani ya kipindi cha chini ya mwezi mmoja, ndoa hiyo ilitikisika na kupeana talaka.

Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu, wawili hao walifunga ndoa tarehe 8 Agosti 2024, katika hafla ya faragha iliyoandaliwa kisiri. Hata hivyo, Toni alifungua rasmi kesi ya talaka ndani ya wiki mbili tu, akidai kwamba ndoa hiyo “haikuwahi kutekelezwa kikamilifu.” Katika nyaraka alizowasilisha mahakamani, alieleza kuwa walitengana tarehe 10 Agosti — siku mbili tu baada ya harusi yao.

Katika hatua ya kushangaza, mwezi Januari 2025, Toni Braxton aliamua kufuta kesi ya talaka na kuiondoa mahakamani. Birdman naye alikubaliana na uamuzi huo, jambo lililomaanisha kuwa kisheria bado ni wanandoa, ingawa hadi sasa hakuna dalili wazi za uhusiano wao kuendelea hadharani.

Kwa muda mrefu, Toni na Birdman wamekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi wa kurudi na kuachana tangu mwaka 2016, na mara kadhaa wamekwepa kuanika maisha yao ya mapenzi hadharani. Mashabiki na wadau wa burudani wanasubiri kwa hamu kujua hatma ya wawili hao maarufu katika tasnia ya muziki.

Hakuna maoni: