Breaking

Alhamisi, 17 Julai 2025

LEO NI SIKU MUHIMU KWA NCHI YETU -RAIS DOKTA SAMIA


 Leo ni siku muhimu na ya kihistoria kwa nchi yetu ambapo tumehitimisha safari tuliyoianza miaka miwili iliyopita kwa kuzindua Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, ikiwa ni mara ya pili kwa Taifa letu kufanya hivi tangu Uhuru. Dira hii ni maoni ya wananchi wote ambapo kwa miaka 25 ijayo wamedhamiria kujenga Taifa jumuishi, lenye ustawi, haki na linalojitegemea.

Tumefikiri wenyewe, tumepanga wenyewe, tumeandika wenyewe na hatua inayofuata ni utekelezaji. Hatua hii inahitaji kila mwananchi kufanya kazi kwa ari, nguvu, maarifa na bidii na kuwepo ushirikiano wa dhati kati ya serikali, sekta binafsi na wadau wa maendeleo. Aidha, hatuna budi kuendelea kudumisha amani, umoja, mshikamano na utulivu nchini ili tufikie shabaha na malengo tuliyojiwekea.

Ninawapongeza wote, hasa wananchi, walioshiriki katika maandalizi ya dira hii, na hivyo kuipa umiliki na taswira ya kitaifa. Mmetimiza wajibu wenu, nami ninawahakikishia kuwa, tumeweza kutekeleza mengi, tutaweza kutekeleza dira hii.



Hakuna maoni: