Breaking

Alhamisi, 10 Julai 2025

MAJINA MATATU YA WAGOMBEA KUPENDEKEZWA LEO NA KAMATI ZA SIASA ZA MIKOA.


Vikao vya Kamati ya Siasa ya Mkoa vinafanyika leo kote nchini kwa ajili ya kujadili na kutoa mapendekezo ya majina ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi walioomba kuteuliwa kugombea Udiwani, Ubunge na Uwakilishi.

Vikao hivyo, vitapendekeza wagombea Udiwani Watatu kwa kila Kata/Wadi, ambao watapigiwa kura za maoni na kuteua pia wagombea Udiwani Viti Maalum Watatu kwa kila nafasi na watapigiwa kura za maoni.

Kulingana na ratiba ya vikao hivyo vya CCM, Kamati hizo za Siasa za Mikoa zitajadili wagombea Ubunge na Uwakilishi na kutoa mapendekezo kwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa-NEC upande wa Tanzania Bara, na kutoa pia mapendekezo kwa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM, Zanzibar.

Tayari, kumeshafanyika vikao vya Kamati za Siasa za Kata, Wadi, vikao vya Kamati za utekelezaji wa UWT, Wilaya, pamoja na vikao vya Kamati ya Siasa ya Wilaya ili kutoa mapendekezo yake kwa Kamati za Siasa za Mikoa.

Aidha, Vikao hivyo vya CCM vinafanyika baada ya kumalizika zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu kwa wanachama za kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Ubunge, Uwakilishi na Udiwani, katika kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu 2025.

Hakuna maoni: