Breaking

Alhamisi, 10 Julai 2025

WAZUNGUMZIA UMUHIMU WA KUIMARISHA BIASHARA YA MIPAKANI NA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU.


Balozi wa Tanzania nchini Msumbuji Hamad Khamis Hamad amekutana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Msumbiji, Maria Benvinda Levy, Jijini Maputo kwa ajili ya kujitambulisha.

Mazungumzo ya viongozi hao, yalielekeza umuhimu wa kuimarisha Biashara ya mipakani na uboreshaji wa miundombinu, hasa kupitia Ukanda wa Maendeleo wa Mtwara; Uwekezaji wa pamoja kwa kuzingatia mazingira bora ya sera na sheria yanayochochea sekta binafsi kushiriki kikamilifu.

Waziri Mkuu Levy, aliahidi kuwa Ofisi yake sambamba na Wizara na Taasisi nyingine za Serikali ya Msumbiji, zitatoa kila aina ya ushirikiano kwa Mhe. Balozi Hamad ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Naye, Balozi Hamad alijitambulisha rasmi kwa Waziri Mkuu Levy na kueleza shukrani kwa mapokezi mazuri pamoja na ushirikiano mzuri kutoka Serikali ya Msumbiji tangu kuwasili kwake. 

Pia alisisitiza dhamira ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuendeleza uhusiano wa karibu kati ya nchi hizi mbili.

Hakuna maoni: