Mcheza mieleka mkongwe Hulk Hogan, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 71.
Hogan ambaye jina lake halisi ni Terry Gene Bollea anaripotiwa kufariki alfajiri ya leo nyumbani kwake Clearwater, Florida, nchini Marekani baada ya kupata mshituko wa moyo.
Polisi wa Clearwater wamesema alikimbizwa hospitalini lakini alitangazwa kufariki muda mfupi baadaye, WWE shirika kubwa la mieleka limetoa taarifa ya masikitiko makubwa na kumwelezea Hogan kama sura ya zama za dhahabu katika mieleka aliyekuwa na mchango mkubwa na aliyeacha alama isiyofutika katika tasnia hiyo.
Katika maisha yake ya ulingo, Hogan alipata mataji mengi ya mieleka na pia alijikita katika filamu na vipindi vya televisheni, akiwahamasisha mashabiki wa michezo hii kote duniani.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni