Mwanamuziki mashuhuri duniani, Rihanna, ameongoza shughuli za mazishi ya baba yake mzazi, Ronald Fenty, yaliyofanyika huko Barbados, katika eneo la Christ Church.
Ibada ya mazishi ilianza kwa kikao cha faragha katika ukumbi wa Garfield Sobers Gymnasium, kabla ya mwili kupelekwa kuzikwa katika makaburi ya Coral Ridge Memorial Gardens, moja ya maeneo maarufu ya makaburi nchini humo.
Marehemu Ronald Fenty alifariki dunia tarehe 31 Mei 2025 kutokana na matatizo ya kiafya ikiwemo kansa ya kongosho, kushindwa kwa mfumo wa upumuaji, na nimonia ya kuvuta vumbi tumboni.
Rihanna, ambaye ni mzaliwa wa Barbados, alihudhuria ibada hiyo akiwa na mpenzi wake A$AP Rocky, pamoja na watoto wao wawili, RZA, mwenye umri wa miaka mitatu, na Riot, mwenye mwaka mmoja. Pia inaripotiwa kuwa Rihanna ni mjamzito na anatarajia mtoto wa tatu.
Mashuhuda wamesema msanii huyo alionekana mwenye huzuni mkubwa, akiwa amevaa mavazi ya heshima ya rangi ya upole, huku akimbeba mwanawe mdogo wakati wa mazishi.
Ingawa uhusiano wa Rihanna na marehemu baba yake haukuwa mzuri katika miaka ya awali, wawili hao waliweza kupatanishwa kabla ya kifo chake.
Mazishi hayo yalihudhuriwa na ndugu wa karibu na marafiki, huku familia ikionekana kugubikwa na simanzi nzito.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni