Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu ya Afya kutoka Wizara ya Afya Dkt.Ona Machangu ametoa wito kwa jamii kuendelea kushirikiana na Serikali katika usambazaji wa vielelezo vya elimu ya Afya ikiwemo shuleni na masokoni vinavyozalishwa na Wizara ya Afya.
Dkt. Machangu ametoa wito huo leo Julai 11, 2025 Jijini Dodoma, wakati akiwasilisha wasilisho la Elimu ya Afya kwenye Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri .
"Moja ya majukumu ya Elimu ya Afya kwa Umma ni kuzalisha vielelezo vyenye maudhui ya elimu ya afya, hivyo niwaombe vielelezo vinaposambazwa katika maeneo mbalimbali kila mmoja ana wajibu wa kuvisambaza vielelezo hivyo," amesema Dkt. Machangu.
Aidha, Dkt. Machangu amesema suala la elimu ya Afya isiwe kwenye masuala ya dharura tu, hivyo ni muhimu kuwa endelevu.
Halikadhalika, Dkt. Machangu amesema elimu ya afya kwa umma imekuwa ikitumia namba namba 199 kwa kupokea maoni ya wananchi kuhusu masuala mbalimbal

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni