Arsenal inajiandaa kuwasiliana na Crystal Palace kujadili iwapo inaweza kumsajili winga wa Uingereza Eberechi Eze bila kuanzisha kipengele cha kutolewa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kwa pauni milioni 68. (Sportsport)
Liverpool imefanya mazungumzo na mshambuliaji wa Crystal Palace Jean-Philippe Mateta, 28. Mfaransa huyo amekutana na wawakilishi wa klabu hiyo mjini Paris. (Footmercato - kwa Kifaransa)
Manchester United imefikia makubaliano na Brentford kumsajili mshambuliaji wa Cameroon Bryan Mbeumo, 25. (UFootball Transfers)

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni