Breaking

Ijumaa, 11 Julai 2025

TETESI ZA SOKA ULAYA- BAYERN YAPELEKA OFA KWA DIAZ.


 Bayern Munich wamewasilisha ofa ya euro milioni 52 (pauni milioni 44.7) kwa ajiliu ya winga wa Liverpool na Colombia Luis Diaz, 28 (Bild).

Nottingham Forest wamekataliwa tena ofa yao kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Brentford Yoane Wissa, 28, ikiaminika kuwa ni chini ya pauni milioni 25 walizowahi kutoa kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Kongo mnamo Januari, Bees wanataka pauni milioni 50 (The Athletic).

Liverpool wako tayari kuanza mazungumzo kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa wa Eintracht Frankfurt, Hugo Ekitike, 23, ingawa klabu hiyo inahitaji kuidhinisha uhamisho wa mshambuliaji wa Uruguay Darwin Nunez, 26, ili kuwezesha dili hilo (Givemesport).

The Reds wamevutiwa na Ekitike lakini bei yake na hali ya mshambuliaji wa Sweden Alexander Isak, 25, huko Newcastle pia inaweza kuwa sababu katika dili lolote (Tbrfootball).

Haraka ya Arsenal ya kumsajili mshambuliaji wa Sweden Viktor Gyokeres, 27, iko hatarini kuvunjika kwa sababu klabu hiyo haijawasiliana na Sporting kwa siku tatu (Abola).

Hakuna maoni: