Breaking

Jumapili, 13 Julai 2025

TETESI ZA SOKA ULAYA: CHELSEA MACHO KWA DONNARUMMA WA PSG

 

Chelsea wana nia ya kumsajili mlinda lango wa Paris St-Germain na Italia Gianluigi Donnarumma, 27. (L'Equipe)

Newcastle wamefufua nia ya kumnunua mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt Mfaransa Hugo Ekitike, 23, na wanatumai kuwashinda Liverpool kwenye usajili wake. (Telegraph)

West Ham wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa zamani wa Aston Villa Douglas Luiz kutoka Juventus, huku Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 27 akiwa ametatizika kufanya vyema kwenye Serie A.

Hakuna maoni: