Rasmi klabu ya wekundu wa msimbazi Simba sc imethibitisha hii leo kuachana na wachezaji kiungo Fabrice Ngoma na golikipa Aishi Manula baada ya wachezaji hao kumalizika kwa mikataba yao hivyo hawatokuwa sehemu kikosi hicho kwa msimu ujao wa 2025/2026.
Ngoma mwenye umri wa miaka 31 raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo alijiunga na Simba sc mnamo Julai mwaka 2023 kwa mkataba wa miaka miwili (2) akitokea klabu ya Al Hilal ya Sudan. Kwa upande wa Aishi Manula alijiunga na Simba sc mwaka 2017 akitokea Azam fc kabla ya kutangazwa tena kujiunga na klabu hiyo ya cha Chamazi, Azam fc kwa msimu ujao 2025/2026 atakuwa sehemu ya timu hiyo.
Wakati huo huo klabu hiyo ambayo makazi yake yako msimbazi imetoa taarifa ya kumtoa kwa mkopo kiungo wao Omary Omary kwenda kuitumikia Mashujaa Fc kwa msimu ujao 2025/2026.
Omary mwenye umri wa miaka 25 mchezaji wa kimataifa wa Tanzania anarejea tena Mashujaa Fc takribani mwaka mmoja tangu ajiunge na Simba sc mnamo 22 Juni 2024.
✍🏾AnoldMathias255



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni