Breaking


Jumamosi, 12 Julai 2025

TETESI ZA SOKA ULAYA: CHELSEA WATAKA DAU LA £100 KWA JACKSON


 Chelsea waweka dau kubwa kwa Nicolas Jackson, Barcelona wamgeukia Marcus Rashford katika kumsaka winga mpya wa kushoto, Juventus wakubali kima fulani kwa ajili ya Jadon Sancho na mengine mengi.

Chelsea imeweka dau la pauni milioni 100 kwa mshambuliaji wa Senegal Nicolas Jackson, 24, huku AC Milan ikimtaka. 

Mchezaji wa Manchester United na Muingereza Marcus Rashford, 27, anafuatiliwa na Barcelona kama winga mpya wa kushoto baada ya klabu hiyo ya Uhispania kushindwa kumnunua mshambuliaji wa Liverpool na Colombia Luis Diaz, 28, na Mhispania mwenye umri wa miaka 22 Nico Williams wa Athletic Bilbao. (Sky Sports)

Hakuna maoni: