Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ametembelea banda la Wizara ya Afya lililopo katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete leo Julai 12, 2025, jijini Dodoma na kupokea maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bi. Roida Andusamile wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri ulioanza Julai 11 hadi 14, 2025.
Dkt. Mpango ameambatana na Waziri wa Nchi OR - TAMISEMI Mhe. Mohammed Mchengerwa, Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama, Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe, Naibu Makatibu wa Wakuu wa TAMISEMI pamoja na Wakurugenzi kutoka Wizara ya Afya.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni