Breaking

Jumanne, 22 Julai 2025

TETESI ZA SOKA ULAYA: MAN UNITED KUMNASA EMI MARTINEZ?


G

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Manchester United wanaangalia uwezekano wa kumsajili Emi Martinez lakini huenda wakakatishwa tamaa na dau la £40 milioni linalotakiwa na Aston Villa kwa kipa huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 32. (Mail)

Winga wa Colombia, Luis Diaz, mwenye umri wa miaka 28, bado ana dhamira ya kuondoka Liverpool katika dirisha hili la usajili wa majira ya kiangazi, na anatumai Bayern Munich watawasilisha tena ofa mpya katika siku chache zijazo ili kujaribu kuishawishi klabu hiyo ya England. (ESPN)

Newcastle wako hatarini kupitwa na Manchester City katika harakati zao za kumsajili James Trafford, kipa wa Burnley na timu ya taifa ya England mwenye umri wa miaka 22. (Telegraph)

Trafford ana hamu kubwa ya kurejea Manchester City majira haya ya kiangazi baada ya City kuingilia kati mpango wa Newcastle wanaotaka kumsajili kipa huyo (Football Insider)

Luis Diaz

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Newcastle wanapanga kumpa Tino Livramento mkataba mpya ili kuzuia nia ya Manchester City, ambao wako tayari kulipa £65 milioni kwa beki huyo wa kulia wa England mwenye umri wa miaka 22. (Times)

Hakuna maoni: