Breaking


Jumatatu, 28 Julai 2025

TETESI ZA SOKA ULAYA : VILLA YAJIUNGA NA MBIO ZA KUMSAKA CALVERT-LEWIN


Aston Villa iko tayari kuchuana na AC Milan na Newcastle katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Dominic Calvert-Lewin, 28, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Everton. (Sun)

Newcastle inatarajia kupokea ofa rasmi kutoka kwa Liverpool kwa ajili ya mshambuliaji wa Sweden Alexander Isak, 25, wiki ijayo. (Mail)

Manchester United imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain na Ufaransa Randal Kolo Muani, 26, ambaye pia anawaniwa zaidi na Juventus. (Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)


#Chanzobbcswahili

Hakuna maoni: