Breaking

Jumapili, 20 Julai 2025

TETESI ZA SOKA ULAYA:JADON SANCHI KUONDOKA MAN UNITED.

 

hatua ya winga wa manchester United na Uingereza Jadon Sancho kutaka kujiunga na klabu ya Juventus kunakaribia kukamilika huku vilabu hivyo viwili vikiwa vimekamilisha baadhi ya maelezo kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Tuttosport - In Italy)

Juventus wako tayari kukubaliana na Manchester United kwa dau la euro 25m (£21.6m) kumnunua Sancho, ambaye yuko katika makubaliano kamili na wababe hao wa Serie A kuhusu kandarasi ya miaka minne yenye thamani ya euro 6m (£5.2m) kwa mwaka. (Sportmediaset - In Italy)

Liverpool wamewasilisha ofa ya £69m pamoja na nyongeza - £78m kwa jumla - kwa mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt mwenye umri wa miaka 23 Mfaransa Hugo Ekitike. (Sky Sports)

Liverpool wanapewa nafasi kubwa ya kumnunua kiungo wa kati wa Crystal Palace na England Adam Wharton, 21, juu ya Tottenham - lakini sio hadi msimu ujao wa joto, kwani mchezaji huyo anataka kukaa mwaka mwingine Selhurst Park. (Sun Sunday)

Barcelona italipa mshahara wote wa mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford wa pauni 325,000 kwa wiki katika mkataba ambao unatarajiwa kumpeleka mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 27 kwa klabu hiyo ya Uhispania kwa mkopo wa awali wa msimu mzima.

Hakuna maoni: