f

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Uhamisho wa Manchester United wa kumnunua mshambuliaji wa Brentford Bryan Mbeumo, 25, umekwama huku klabu hiyo ya London ikiongeza bei yao hadi kufikia £70m, huku United hawataki kulipa zaidi ya £65m. (Guardian) 

Liverpool wameanza mazungumzo na Eintracht Frankfurt kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Hugo Ekitike, 23. (Sky Sports), 

Hata hivyo, Newcastle United wanasonga mbele na jaribio lao la kumsajili Ekitike kwa matumaini ya kumpanga pamoja na mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 25, msimu ujao. (Telegraph - subscription required)

g

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Aston Villa ni miongoni mwa klabu za Ligi ya Primia zinazopania kumnunua winga wa Manchester United na Argentina Alejandro Garnacho, 21. (Mail) 

Manchester United wanavutiwa na mchezaji wa Chelsea Nicolas Jackson, 24, huku Aston Villa na AC Milan pia wakifuatilia hali ya mshambuliaji huyo wa Senegal. (Time- subcription required)