Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dokta Samia Suluhu Hassan, imeendelea kufanya mageuzi kwenye upande wa mazao ya biashara.
Chini ya mageuzi hayo, uzalishaji wa mazao ya biashara umeongeza thamani ya mauzo ya kilimo nje ya nchi kwa asilimia 67 kutoka Dola za Marekani Bilioni-2.1 mwaka 2021 hadi Dola za Marekani Bilioni-3.5 mwaka 2024.
Aidha, mauzo ya Korosho nje ya nchi yamepaa zaidi huku uongezaji wa thamani ya Korosho zinazozalishwa umetajwa kuwa sababu ya kupaa kwa mauzo ya zao hilo katika masoko ya nje.
Mwaka 2024, thamani ya mauzo ya Korosho nje ya nchi ilikuwa dola Milioni-541 ikilinganishwa na dola milioni-206 mwaka 2023, sawa na ongezeko la asilimia 162.
Hii ilitokana na kuongezeka kwa kiasi cha korosho kilichouzwa nje kwa asilimia 95 na kufikia tani 428,300 mwaka 2024 ikilinganishwa na tani 219,600 zilizouzwa mwaka 2023.
Hali hii inaonesha namna gani Serikali ya awamu ya sita ilivyoweka jitihada katika suala la bei ya mazao ili kumkwamua zaidi mkulima nchini.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni