Chama Cha Mapinduzi(CCM,kimetangaza tarehe mpya ya uteuzi wa mwisho wa wagombea wa nafasi za ubunge,uwakilishi na udiwani ndani ya CCM,Julai 28,Mwaka huu na kuwataka wagombea kuwa watulivu wakati michakato ikiendelea.
Mchakato wa uteuzi utafanyika kupitia kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM),Jijini Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma,Katibu wa NEC,Itikadi,Uenezi na Mafunzo,CPA Amos Makalla amesema kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM,NEC, kitakutana Julai 26,Mwaka huu kikitanguliwa na vikao vingine.
CPA Makalla amesema maandalizi ya vikao hivyo yanaenda vizuri na ratiba imebadilika kutokana na idadi kubwa ya wagombea waliojitokeza na chama kinataka kitende haki.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni