Breaking

Jumapili, 20 Julai 2025

WATENDAJI WA VYOMBO VYA HABARI VYA CCM WAKUTANA KUIMARISHA UTENDAJI NA USHIRIKIANO


Watendaji Wakuu wa vyombo vya habari vya Chama cha Mapinduzi (CCM) wamekutana katika kikao cha kutathmini utendaji wa majukumu yao na namna ya kuendeleza ushirikiano miongoni mwao.

Kikao hicho kimefanyika jijini Dar es salaam na kuongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Uhuru Media Group(UMG) Dennis Msacky, chombo kinachounganisha vyombo hivyo huku akisisitiza utaratibu huo kuwa wa mara kwa mara kuimarisha utendaji na ushirikiano miongoni mwa vyombo hivyo.

Katika kikao hicho Mtaalam wa masuala ya Biashara Prof. Marcelina Chijoriga, alialikwa kutoa elimu kuhusu namna vyombo hivyo vinavyoweza kujiendesha kisasa zaidi.

Aidha, washiriki wamekubaliana kwamba vikao vya aina hiyo vinafaa kuwa endelevu kuhakikisha ufanisi unaongezeka katika majukumu pia kufikia malengo ya kuanzishwa kwa vyombo hivyo.

Watendaji wa vyombo vya habari waliokutana ni kutoka Africa Media Group Ltd, Uhuru Media Group Ltd,    Uhuru Publications Ltd na Radio Uhuru Fm.

Hakuna maoni: