Breaking


Jumamosi, 23 Agosti 2025

BENKI YA NMB YASHIRIKI SELOUS MARATHON 2025



Benki ya NMB imeendelea kuthibitisha dhamira yake ya kuunga mkono michezo na afya za Watanzania kwa kushiriki kikamilifu katika Selous Marathon iliyofanyika mkoani Morogoro.



Kwa kauli mbiu ya “Tumekupata”, vilima vya Morogoro vimeshuhudia wafanyakazi wa NMB wakijitokeza kwa wingi, wakiongoza mstari wa mbele katika kujenga afya ya mwili na akili. Ushiriki huu ni sehemu ya utamaduni wa benki kuhakikisha wafanyakazi wake wana afya bora ili waendelee kuhudumia wateja kwa ueledi, ubunifu na weledi wa hali ya juu.



Katika mbio hizi, wafanyakazi walijipima kwa umbali tofauti—kila mmoja akijiuliza kwa tabasamu: “Leo kilomita zimesoma ngapi?”



Kwa NMB, afya na michezo ni zaidi ya burudani; ni msingi wa kuwahudumia wateja wake kwa karibu na kwa moyo wote.


#NMBKaribuYako


Hakuna maoni: