Breaking


Jumatatu, 4 Agosti 2025

𝐊𝐀𝐑𝐈𝐁𝐔𝐍𝐈 𝐍𝐀𝐍𝐄𝐍𝐀𝐍𝐄 – 𝐓𝐔𝐎𝐍𝐉𝐄 𝐀𝐒𝐀𝐋𝐈 𝐘𝐀 𝐔𝐑𝐈𝐓𝐇𝐈 𝐖𝐄𝐓𝐔

 

Katika mabanda yetu ya TFS yaliyosambaa katika kanda zote za Nanenane, tunakukaribisha upate fursa ya kipekee ya kuonja Misitu Honey — asali halisi ya Tanzania, inayozalishwa kwa kiwango cha ubora usio na shaka.

Lakini hii si asali tu kama unavyoifahamu. Ni urithi wa tiba, chakula bora, uzuri wa ngozi, na heshima katika familia. Wananchi wanaotembelea banda letu hupewa:

✅ Elimu ya matumizi ya asali kama tiba ya asili na kinga ya mwili

✅ Jinsi ya kutambua asali feki na orijino

✅ Fursa ya kuonja bure na kununua bidhaa bora za nyuki

✅ Maarifa ya matumizi ya bidhaa za nyuki katika urembo na heshima ya ndoa


Tembelea mabanda ya TFS katika mikoa yote yenye maonesho ya Nanenane

Jifunze, onja, nunua na shiriki katika safari ya uhifadhi wenye faida kwako na kwa Taifa.

Hakuna maoni: