MGOMBEA Urais kupitia Chama ChaMapinduzi(CCM),Rais Dokta Samia Suluhu Hassan,ameahidi kuendeleza ujenzi wa miundombinu ya barabara wilayani Chamwino kwa kujenga kilomita kumi kwa kiwango cha lami na kuimarisha barabara kwa kiwango cha changarawe
Dokta Samia ametoa ahadi hiyo leo katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Wilaya ya Chamwino,Mkoani Dodoma ambapo pia ameahidi kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa kuhakikisha Chamwino yote yanapatikana maji ya uhakika.
Amesema Jimbo la Rais halitakiwi kuwa na shida yoyote ile hivyo wakimchagua atahakikisha anaendeleza kazi nzuri aliyoianza na kumaliza changamoto zote zilizopo.
Upande wa afya amesema ataongeza vituo vya afya 10 na Zahanati nyingine tano.
Jioni Rais Samia atakuwa na mkutano mkubwa wa hadhara katika uwanja wa Tambukareli Jijini Dodoma.






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni