Breaking


Jumapili, 31 Agosti 2025

HISTORIA IMEANDIKA KASARANI STADIUM 🏟️

Mwimbaji nyota kutoka Tanzania, Zuchu, ameweka historia usiku wa jana baada ya kutoa burudani ya aina yake katika mchezo wa fainali za CHAN 2024 uliofanyika kwenye Uwanja wa Kasarani, Nairobi  Kenya.


Zuchu, ambaye ni miongoni mwa wasanii wanaowakilisha vyema muziki wa kizazi kipya kutoka Afrika Mashariki, aliteka nyoyo za maelfu ya mashabiki waliokuwa wamefurika uwanjani. Mashabiki walijawa na shangwe na nderemo huku wakicheza na kuimba naye nyimbo zake maarufu zilizotikisa Afrika na duniani.


Burudani hiyo iliipa ladha ya kipekee fainali hizo, ambazo zilihudhuriwa na wageni mashuhuri, viongozi wa michezo, pamoja na mashabiki kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika.

Tukio hili linaonesha namna muziki na michezo vinavyoweza kuunganisha watu, huku Zuchu akionesha hadhi ya juu ya muziki wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.




#CHAN2024 | #Zuchu | #Kasarani


Hakuna maoni: